Saturday, 17 February 2018

Wanajeshi wa Rwanda waua wenzao wa DR CongoWANAJESHI watano wa DR Congo wameuawa na wanajeshi wa Rwanda kulingana na taarifa kutoka kwa jeshi la nchi hiyo
JENERALI  Bruno Mandevu amesema vita vimezuku katika mbuga ya wanyama ya Virunga katika ardhi ya Congo , madai ambayo Rwanda imekana.
Amesema wanajeshi wa Congo walidhania kwamba walikuwa wakikabiliana na waasi waliopo katika eneo hilo.
Wengine wanahofia kwamba mapigano huenda yakaongeza hali ya wasiwasi iliyopo kati ya mataifa hayo mawili ambayo yana historia mbaya. Rwanda iliwavamia mara mbili majirani zake Congo mwaka 1990.
Msemaji wa jeshi la Rwanda, kanali Innocent Munyengango amethibitisha kutokea mashambuliano hayo na kusema kuwa hakukuwa na majeraha upande wa Rwanda.
''Jeshi la Congoleese lilivamia kambi yetu na kutushambulia. Wanajeshi wetu walilazimika kujitetea'', amesema.
Mashariki mwa taifa la DR Congo karibu na mpaka na Rwanda ni eneo ambalo limekuwa halina udhibiti.
Mashirika ya misaada yanaonya kutokea kwa ghasia katika mkoa wa Ituri uliopo Kaskazini mashariki, ambapo Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linasema zaidi ya watoto 46,000 wametoroka.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga ameona vijiji vilivyochomwa katika mkoa huo ambapo watu kutoka makundi ya Hema na Lendu wamekuwa wakipigania udhibiti.
Mapema wiki hii, Baraza la wakimbizi nchini Norway limeonya kwamba mzozo nchini DR Congo unakaribua kutibuka.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, watu zaidi wameachwa bila makazi nchini hapa kuliko nchini nyingine yoyote. Watu milioni 4.5 wanahitaji msaada.
Chanzo cha habari BBC


No comments:

Post a Comment