Thursday, 8 February 2018

Zijue njia tano za kukabiliana na miguu kuwaka motoMguu wenye maumivu

KAMA vilivyo viungo vingine katika mwili wa binadamu, mguu au miguu ni kiungo muhimu ambacho kinamwezesha kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kutokana na umuhimu huo, mtu anapougua miguu anakuwa katika wakati mgumu kwa kuwa hawezi kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa haraka na hivyo kumfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufasaha

Yapo magonjwa mengi ya miguu, kama magoti kuvimba au kujaa maji, kuuma mguu mzima kwa ujumla au maumivu ya miguu kama inawaka moto.

Mara nyingi maradhi ya miguu kuwaka moto yanawapata watu ambao shughuli zao zinawalazimu kutembea umbali mrefu huku wakitumia muda mwingi. Pia wale wanaokaa kwa muda mrefu huku miguu yao ikiwa imening'inia.

Miguu na nyayo kuuma kama vinawaka moto inasababishwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu na ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitajika ndani ya mwili kwa kuwa chakula kinachotumiwa hakifai kwa afya bora.

Chakula cha asili kinahitajika zaidi kuondoa sumu zinazoleta athari hizo ndani ya mwili pamoja na kufanya mabadiliko katika aina ya vyakula vitakavyoliwa kwa ajili ya kupata virutubisho na madini muhimu.

Unaweza kuondokana na tatizo hilo kwa kutumia vyakula, matunda na maji kwa kuzingatia maelekezo.

Maji ya uvuguvugu na chumvi
Ukiwa umekaa tumbukisha miguu yako ndani ya maji ya uvuguvugu yaliyoongezwa chumvi ya mawe yakiwa ndani ya karai kwa muda wa nusu saa. Wakati huo osha sehemu ambazo hazijaguswa na maji hayo hadi magotini.

Limau
Osha miguu na nyayo kwa maji moto na sabuni, kata limau katika vipande viwili, paka sehemu zote unazojisikia maumivu.

Msubili
Osha miguu na nyayo kwa maji moto na sabuni, ponda jani la msubili, paka sehemu zote unazojisikia maumivu

Viazi mviringo
Osha miguu na nyayo kwa maji moto na sabuni, suuza kwa maji baridi, kisha paka kwenye sehemu zote zenye maumivu ujiuji wa viazi mviringo ambao umesha uponda , baada ya saa moja osha miguu kwa maji baridi.

Methi
Loweka ndani ya maji nusu kilo ya mbegu za methi, baada ya kuvimba zianike  kwenye jua hadi zikauke vizuri, kisha saga na kupata unga laini ambao utachanganya kijiko kimoja cha mezani ndani ya nusu glasi ya maji kisha paka miguu utaondokana na tatizo hilo.

Kwa mwenye tatizo hilo na mengine ya kiafya anaweza kuja makao makuu yetu Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Abdallah Mandai kwa ushauri wa namna ya kutumia virutubisho na mimea katika kukabiliana na matatizo ya maradhi mbalimbali.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800 au dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.
No comments:

Post a Comment