Tuesday, 20 February 2018

Zingatia kufanya moja ya mambo haya kutibu sekenene


SEKENENE ni ule ugonjwa ambao kipele kinajitokeza katika kope za macho na kusababisha maumivu makali. Ni aina ya kijipu.
Unapokumbwa na tatizo hili unaweza kutumia sandali, wali, pete ya dhahabu na karafuu kukabiliana nalo.

Sandali

Sugua sandali nyekundu kwenye jiwe safi baada ya kuweka maji, baadaye tengeneza ujiuji unaotokana na unga huo kisha upake kwenye sekenene. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku nne.

Wali

Chukua wali uliopashwa moto vizuri weka ndani ya kitambaa kisafi kisha kanda kwenye sekenene.  Fanya hivyo mara kwa mara hadi unapobaini umepona.

Pete ya dhahabu

Sugua pete ya dhahabu kwenye ngozi ya mwili hadi ipate joto, ikandamize kwenye sekenene. Fanya hivyo mara nyingi iwezekanavyo wakati wa asubuhi, mchana na jioni kwa muda wa siku nne utapata nafuu au kupona kabisa.

Karafuu

Chukua karafuu kile kichwa chake kiloweshe, kikilainika sugua nacho polepole pale unapoonekana mdomo wa sekenene, baada ya muda mfupi ama siku moja kitatoweka (kupona).

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.No comments:

Post a Comment