Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akiwa ameshika mmea maarufu kwa jina la gole ambao unatibu maradhi mbalimbali ikiwemo kuhara na kidonda kibichi. Inashauriwa mtu asiutumie mmea huu bila kupata maelekezo kutoka kwa mtaalam kwa sababu za kitabibu.
KUHARA ni kujisaidia kinyesi chenye maji maji mara kwa mara. Tatizo hilo linatokea baada ya utumbo mdogo kushindwa kuhifadhi kiasi kikubwa cha maji katika mwili wa binadamu.
Baadhi ya
sababu zinazoweza kusababisha mtu kuharisha ni kula kupita kiasi, kula
mchanganyiko wa vyakula vingi, woga, wasiwasi, haraka, kuchacha chakula ndani
ya tumbo, kula chakula kisichofaa (sumu bacteria, virusi, vijidudu) au vimelea
ndani ya chakula.
Utumbo mdogo
una uwezo wa kupokea zaidi ya lita nane za maji kwa siku kutoka kwenye vyakula
au vinywaji vinavyopitia mdomoni na maji mengine kutoka sehemu mbalimbali za
mwili.
Inapotokea
kunakuwa na maji mengi zaidi katika utumbo mdogo yanashindwa kutoka mwilini kwa
njia ya kawaida kama kupitia mkojo na jasho, basi maji hayo hutelemka katika
utumbo mkubwa ambao hauna uwezo wa kuyatunza.
Wingi huo wa
maji ndiyo unaopelekea mtu kuanza kuhara. Tatizo hilo linaweza kutibiwa kwa
mimea na matunda tunavyovitumia kila siku ambavyo ni mkaa/majivu, embe bichi,
mbegu ya embe, mizizi ya mpera, bizari, karela asali/nazi, mung’unya na ukoko
wa wali.
Mkaa au majivu
Unaweza
kutumia mkaa wowote, ila mkaa wa makaratasi, kifuu cha nazi, mkuyu, na
msonobari unafaa zaidi. Chukua kijiko kimoja cha unga laini wa mkaa, weka
katika glasi moja ya maji moto, koroga vizuri na kunywa baada ya maji kuwa vugu
vugu. Kunywa mara tatu kwa siku muda wa siku tatu.
Embe bichi
Tumia embi
bichi lilichanganywa na pilipili manga na asali, usile zaidi ya embe mbili kwa
siku, endelea na tiba hii kwa muda wa siku tatu.
Mbegu za
embe
Chukua nusu
kijiko cha chai cha mbegu zilizokaushwa katika kivuli, weka ndani ya nusu glasi
ya maji, ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asali koroga vizuri na kunywa,
tumia dawa hii mara tatu kwa siku tatu.
Mizizi ya
mpera
Kausha
magamba ya mizizi ya mpera, saga ili kupata unga laini, chukua kijiko kimoja
cha chai cha unga huo, ongeza kingine cha mezani chenye asali koroga vizuri na
kunywa. Tumia dawa hii mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu.
Bizari
Chukua
kijiko cha chai cha bizari mbichi iliyopondwa au unga wa bizari iliyokaushwa na
kusagwa. Changanya katika glasi moja ya maji au maziwa kunywaji. Tumia dawa hii
mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tatu.
Karela (asali,
nazi)
Tengeneza
juisi ya karela mbili, ongeza kijiko kimoja cha asali, changanya na maji ya
dafu moja dogo, kunywa yote mara moja. Tumia dawa hii mara tatu kwa siku muda
wa siku tatu.
Mung’unya
Tengeneza
juisi ya mung’unya, ongeza chumvi kiasi cha kuifanya isikike unapoionja, kunywa
glasi moja asubuhi na nyingine jioni kwa muda wa siku tatu.
Ukoko wa
wali na maziwa
Kausha ukoko
wa wali ulioungua na saga ili kupata unga laini. Hii ni tiba ya mtoto
anayeharisha, chukua kijiko kimoja cha unga katika glasi moja ya maziwa, mpe
robo glasi ya mchanganyiko huo kila baada ya nusu saa.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na
Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.
Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la
kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam
au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali
vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.
Mtaalamu Mandai anapatikana
kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:
Post a Comment