Saturday, 17 February 2018

Zingatia moja ya mambo haya kuondokana na kwikwi
Mtaalamu wa tiba, tishe na virutubisho, Abdallah Mandai akifafanua jambo wakati akizungumzia namna ya kuondokana na tatizo la kwikwi.


KUPIGA kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara nyingi husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu. Kitaalamu kwikwi inatokea baada ya hewa kuingia kwenye mapafu ghafla.

Hata hivyo, kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kuzuia kwikwi ambazo ni pamoja na kutumia kikonyo cha nyonyo, kumtia hofu mgonjwa, maji baridi, kuzuia pumzi, sukari, iriki na mnanaa.

Kikonyo cha nyonyo
Jaza maji baridi katika kikonyo cha nyonyo, kunywa kidogodogo kwa muda wa dakika tatu hadi 10, utaondokanana na hali hiyo au kuisha kabisa.

Hofu
Fanya kitu ambacho kinaweza kumwogopesha au kumshtusha mgonjwa wa kwikwi. Kwa kawaida baada ya tendo hilo kwikwi hukoma.

Maji baridi
Chukua glasi ya maji baridi ongeza kijiko kimoja cha chai cha asali, kisha koroga vizuri, kunywa polepole lakini mfululizo hadi maji yote yaishe utaona nafuu kubwa au kuisha kabisa hali hiyo.

Kuzuia pumzi
Mzibe pua au kumzuia pumzi mgonjwa wa kwikwi kwa muda mrefu iwezekanavyo, ataondokana na tatizo hilo baada ya tendo hilo.

Sukari
Wakati ukiwa umeshinikiza shingo kushoto na kulia kwa vidole gumba vya mikono, lamba sukari kidogo iliyojaa kwenye kijiko cha chai hadi iishe. Baada ya hapo utapata nafuu ya tatizo lako.

Iriki na mnanaa
Pia unaweza kuponda iriki tatu pamoja na majani matano ya mnanaa, chemsha katika glasi moja ya maji, baada ya kupoa kunywa polepole hadi iishe utaona umeondokana na hali hiyo.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment