Monday, 12 February 2018

Zuma kung’oka leo?


    Jacob Zuma
Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama hicho kinafanya uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya Rais Jacob Zuma.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.
Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.
Bwana Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.
BBC


No comments:

Post a Comment