Thursday, 8 March 2018

Adaiwa kutiwa mbaroni kwa kujifanya mwenyekiti


Dk Titus Kamani

Mary Meshack, Dodoma

MWENYEKITI wa Chama cha Ushirika cha Morogoro Famers Coperative Union (MOFACU), cha mkoani Morogoro, Pascal Madunga anashikiliwa na jeshi la Polisi mkaoni Dodoma kwa kosa la kujiweka madarakani kwa nafasi hiyo kinyume cha sheria.

Madunga amekamatwa na jeshi hilo kwa amri ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika,  baada ya tume hiyo kujiridhisha kuwa hana uhalali wa nafasi hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa tume hiyo, Dk.Titus Kamani amesema,Tume imefikia uamuzi wa kumkamata mwenyekiti huyo baada ya kubaini baadhi ya vyama kuchukulia utani katika uendeshaji wa vyama
hivyo na kujaribu kufanya ujanja ujanja na kujipa nafasi za uongozi.

“Sasa Tume imeibani Mwenyeiti anayewakilisha MOFACU si kiongozi halali na atabaki kwa vyombo vya dola ili tujue uhalali wake wa kujiita mwenyekiti na tujue waliomchagua.”alisema Dk.Kamani na kuagiza askari wamchukue na kumweka chini ya ulinzi

Amesema,kukamatwa kwa Madunga ,iwe salamu kwa watu wengine wenye tabia hiyo huku akisema,haiwezekani kikundi cha watu wachache wakajimilikisha chama kwa kujifanya wao ni viongozi wakati hawakuchaguliwa na wanachama wa chama husika.

No comments:

Post a Comment