Sunday, 25 March 2018

Ajali ya Hiace yaua 24 mkoani Pwani

WATU 24 wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Hiace lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda wilaya ya Mkuranga, mkoanini Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 25, 2018 eneo la Mparanga wilayani Mkuranga.

Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment