Thursday, 22 March 2018

Baada ya kimya kingi Lipumba aibuka kuunga mkono jitihada za serikaliRais Dk John Magufuli (kulia) akipeana mkono na Prof. Ibrahim Lipumba (PICHA YA MAKTABA)

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema anaunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli katika mpango wa ukusanyaji kodi, huku akitaka utekelezaji huo uzingatie uhalisia.

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari baada ya ukimya wake wa muda mrefu na kusema Baraza Kuu linaitaka mamlaka inayohusika na masuala ya ukusaji kodi kwa wafanyabiashara iwe inatoa makadirio mazuri yanayowezesha kuwapa fursa wateja wao kulipa kodi vizuri.

“Baadhi ya kampuni na wafanyabiashara wanakadiriwa kodi kubwa kuliko wanachouza na hatimaye biashara zao zinafungwa. 

“Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitaka serikali ifanye makadirio ya kodi ambayo yatakuwa yanazingatia hali halisi, mamlaka ya kodi isiwakamue wafanyabiashara hadi biashara kufungwa na kusababisha kupata hasara,” amesema Prof. Lipumba.

Kwa upande mwingine, Prof. Lipumba amedai Baraza kuu limepata kuwepo kwa malalamiko ya hali ya maisha kuwa magumu kupitiliza na kuiomba serikali iongeze mzunguko wa fedha ili kuinua maisha ya watanzania wa hali ya chini.

No comments:

Post a Comment