Monday, 26 March 2018

Baada ya vita vya kibiashara vya Trump China yaonya kutetea maslahi yake dhidi ya Marekani


Rais Donald Trump
CHINA imeionya Marekani kwamba itatetea maslahi yake kuhusu biashara kulingana na chombo cha habari cha China baada ya rais Donald Trump kuwekea ushuru bidhaa za China.
Matamshi hayo yanajiri katika simu kati ya makamu wa chama tawala cha China Liu He na Waziri Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin. Trump ametangaza mipango ya kuziwekea ushuru wa hadi Dola za Marekani bilioni 60 bidhaa za China ikiilaumu nchi hiyo kwa wizi wa ubunifu.
Hatua hiyo imesababisha wasiwasi katika soko la hisa na hofu ya kuzuka kwa vita vya kibiashara. Liu ambaye ni mshauri mkuu wa maswala ya kuuchumi wa rais Xi Jinping aliambia Mnuchin kwamba Beijing iko tayari kutetea maslahi yake ya kitaifa lakini ikatumai kwamba pande zote mbili hazitakuwa na upendeleo na kufanya kazi pamoja kulingana na chombo cha habari cha Xinhua.
Wakati wa mazungumzo ya simu, ambayo yanadaiwa kuwa ya ngazi ya juu kati ya serikali hizo mbili tangu rais Trump kutangaza ushuru huo siku ya Alhamisi wiki iliyopita, Liu pia aliishutumu Marekani kwa kukiuka sheria za kimataifa baada ya uchunguzi wake kuhusu hatua ya China kuigiza utengezaji wa bidhaa zake.
Huku kukiwa na wasiwasi kuhusu biashara, mkurugenzi mkuu wa shirika la kibiashara duniani WTO Roberto Azevedo ameonya kuwa vikwazo hivyo vipya vya kibiashara vitaathiri uchumi duniani. Trump hata hivyo amesema hatua ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China imeanza kuzaa matunda.
Mataifa mengine yameanza kujadiliana mikataba yenye usawa na Marekani , rais huyo alisema siku ya Ijumaa.
Baada ya hatua hiyo ya rais Trump, China imesema ilikuwa inapanga kulipiza kisasi kupitia vikwazo vya ushuru dhidi ya Marekani wa thamani ya dola blioni 3, ikiwemo ushuru dhidi ya bidhaa za kilimo pamoja na aliminium.
Beijing imeionya Marekani kwamba haiogopi vita vya kibiashara. lakini ikasema kuwa inatumai kuzuia vikwazo hivyo kupitia majadiliano.

No comments:

Post a Comment