Wednesday, 14 March 2018

Baraza la Wazee Chadema lamwangukia JPMMwandishi Wetu
BARAZA la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeomba kukutana na Rais John Magufuli ili kushauriana masuala mbali mbali yanayolihusu taifa ikiwemo uchumi na usalama.
Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka kwenye mkutano wao na wanahabari amesema taifa linapita katika kipindi kigumu na majaribu makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, hivyo ni lazima viongozi wachukue hatua ya kusikilizana.
"Rais Magufuli ambaye ni mzee mwenzetu, aongozwe na busara za kiuongozi na hekima za uzee, akubali kuitikia wito wetu wa kukutana naye katika kikao cha pamoja ambacho tutakuwa na ujasiri wa kumwambia ukweli na kumshauri,” amesema.
Katika hatua nyingine baraza hilo limeshangazwa na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa kijana Abdul Nondo alijiteka wakati Jeshi la Polisi linasema linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment