Thursday, 29 March 2018

Bonanza la Pasaka kutimua vumbi Ukonga Magereza


Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana

Suleiman Kasei

BONANZA la Tamasha la Sikukuu ya Pasaka linatarajiwa kutimua vumbi kuanzia leo hadi Jumapili Aprili Mosi mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, kilichopo Ukonga Dar es Salaam zamani kikifahamika kama Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza, Ukonga.

Akizungumzia kufanyika kwa Bonanza hilo, Mkuu wa Chuo hicho, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana, amesema  kufanyika kwa  tamasha hilo ni mwendelezo wa wanamichezo Tanzania Bara na wale wa Zanzibar kualikana kila mwaka.

Naibu Kamishna Nkana amesema mashindano hayo ya ujirani mwema yanafaanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu yanafaanyika Tanzania Bara.

Nkana amefafanua kuwa bonanza hilo linashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, wavu na mingine mingi.

“Hii ni zamu ya wanamichezo kutoka upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara kwa  ajili ya kushiriki,” amesema.

Ameongeza kuwa ratiba ya mwaka huu imepangwa kuanza leo ambapo mataraajio yao ni kuona ushindani mkubwa katika bonanza hilo.

“Kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu, wavu, pete, kikapu, riadha, kuvuta kamba, mbio za magunia na kufukuza kuku, bao na draft.

"Ni bonanza la wazi la siku tatu kuanzia leo hadi Aprili Mosi ambalao litashirikisha michezo mbalimbali katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya  Urekebishaji hapa Ukonga, Dar es Salaam.

"Tumeandaa michezo mingi ili kuongeza maana halisi ya tamasha la michezo baina yetu, hivyo ni burudani tosha  kwa watakaoshiriki na watakaohudhuria, huku tukiamini ya kwamba  michezo ni furaha na afya," amesema Nkana.

No comments:

Post a Comment