Friday, 30 March 2018

CAG aomba radhi adai alikosea taarifa yake kuhusu deni la taifa


Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, Profesa. Mussa Assad akimkabidhi Rais Dk. John Magufuli ripoti hiyo ya ukaguzi ya mwaka 2016/17. 

Peter Simon 

MDHIBITI na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, Profesa. Mussa Assad amewaomba radhi wananchi na serikali kuhusu taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi, deni hilo ni himilivu.

Prof. Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma jana ambapo amesema deni halisi ni sh. trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.

CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa, Rais Dk. John Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la taifa alisema kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa bungeni. 

No comments:

Post a Comment