Sunday, 11 March 2018

Chama tawala China chaidhinisha ‘rais wa maisha’


Rais Xi Jinping
CHAMA tawala cha National People's Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengele cha Katiba na kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika hapo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.
Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.
Chama hicho kinasema mabadiliko hayo yataupa nguvu na kuboresha mfumo wa uongozi nchini humo.
Yeyote anayepinga mabadiliko hayo, kwa hofu kuwa itampa nguvu zaidi mtu mmoja, amezimwa nchini humo.
Wanahabari walinyimwa idhini ya kuingia Bungeni, kushuhudia mchakato wa kupiga kura hiyo.


No comments:

Post a Comment