Tuesday, 27 March 2018

Deni la taifa lapaaRais Dk. John Magufuli akipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2016/17 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad iliyobainisha madudu serikali za mitaa na mashirika ya umma.

Peter Simon

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG), Profesa Mussa Assad amesema deni la Taifa linatia wasiwasi hivyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wake.

Profesa Assad ametoa kauli hiyo leo (Jumanne Machi 27, 2018) na kubainisha kuwa  deni hilo ni sh. Trillion 46 kutoka sh. Trillion 41 la mwaka uliopita, kwamba ni ongezeko la asilimia 12.

Alikuwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji ripoti yake ya ukaguzi mwaka 2016/17 iliyobaini madudu Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni, tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) siyo mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza  ku-control ukuaji wa deni hilo,” amesema.

No comments:

Post a Comment