Sunday, 18 March 2018

Dk Mwigulu awafunda wanafunzi kuachana na harakatiDk. Mwigulu Nchemba 

WAZIRIwa Mambo ya ndani, Dk. Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya kwa serikali badala yake wawe na mitazamo chanya.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kongamano la Unilife lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.

Amesema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwa kuwa haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la chifu, majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za taifa ambazo niliona hazina manufaa,” amesema Dk. Mwigulu.

Amesisitiza kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya serikali bila kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.

“Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya bali kuwa na mitazamo chanya na ukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro,” amesema.


No comments:

Post a Comment