Sunday, 18 March 2018

Fahamu namna ya kukabiliana na maradhi ya kifafa


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akielezea namna kutumia tiba tajwa kukabiliana na kifafa.

UGONJWA wa kifafa kwa lugha nyingine unaitwa ugonjwa wa kuanguka. Ni tatizo kubwa, mara nyingi linawakumba watoto na watu wazima pia. Waweza kumuanza mtoto akiwa mdogo au mwanzo wa umri wa utu uzima.

Zipo aina mbili za kifafa zinazojulikana kitaalam kama pept mal na grand mal (kifafa kikuu). Pept mal kinapomkumba mgonjwa anapigwa kifafa muda mfupi tu mara anarudia fahamu zake haraka. Mtu anakumbwa huku akijijua kinachoendelea.

Lakini katika kifafa kikuu huteka ubongo wote hata macho hubadilika, povu hutoka mdomoni huku akisaga meno.

Chanzo cha kifafa ni hitilafu katika mishipa ya fahamu hasa chembe ya ubongo. Ila katika kifafa kikuu ni hitilafu kubwa zaidi ya ubongo kama mshtuko mkubwa ubongoni, majeraha ubongoni na magonjwa kama uti wa mgongo, homa ya matumbo na sumu sugu ya kilevi.

Unaweza kutibu kifafa kwa kutumia zabibu mbivu, mlonge, mpera, karoti, tango na letuce.

Zabibu mbivu

Tengeneza nusu lita ya juisi ya zabibu kunywa yote kutwa nzima, fanya hivyo kila siku katika kipindi cha mwezi mmoja.

Karoti na tango

Pata nusu lita ya juisi mchanganyiko wa karoti na tango kunywa kila siku kwa muda wa miezi mitatu.

Mlonge

Chemsha mzizi mchanga wa mti wa mlonge, kunywa glasi moja mara mbili kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu.

Mpera

Chemsha ndani ya lita moja ya maji majani ya mpera kiganja kimoja kwa muda wa dakika 10, kunywa glasi moja mara mbili kutwa kwa muda wa miezi mitatu.

Letuce

Chukua mboga ya letuce mbichi kamua juisi yake na kuitumia glasi moja mara mbili kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu

Indian coral tree: (Mjafari)

Majani ya mti huu ni muhimu sana kudhibiti na kutibu degedege kwa watoto ambao ukubwani inaweza kugeuka kuwa kifafa. Kunywa juisi yake glasi moja mara mbili kutwa kwa muda wa miezi mitatu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment