Monday, 5 March 2018

Fanya haya unapobaini umeathirika na maradhi ya iniKUSINYAA kwa ini ni ugonjwa unaotokea baada ya makovu magumu kuzingira ini na hivyo chembechembe laini kufanya ini lionekane kama sponji.

Ini linapokuwa limeathirika namna hiyo, hushindwa kufanya kazi zake kama kutengeneza protini na kuondoa sumu mwilini. Ugonjwa huu pia unaweza kusababisha mkusanyiko wa maji ndani ya tumbo hivyo kumfanya mgonjwa kuvimba.

Kuathirika kwa ini kunaweza kutokana na unywaji wa pombe kuzidi kiasi, uvutaji wa hewa na ulaji wa chakula chenye sumu na ugonjwa wa manjano.

Baada ya ini kuathirika kwa ugonjwa wa kusinyaa haliwezi kutibiwa na kurudi katika hali ya awali, ila mgonjwa anaweza kupata nafuu kwa kuzingatia kula chakula kinachofaa na kuacha kila aina ya kileo.

Hata hivyo,  zipo aina nyingi za tiba zinazosaidia kupunguza athari za ini ambazo ni pamoja na mbegu za papai na ndimu, zambarau, mchunga, msubili,  chumvi, nyanya na pilipili manga.

Mbegu za papai na ndimu

Chukua juisi ya mbegu za papai kijiko kimoja cha mezani changanya na matone kumi ya juisi ya ndimu. Kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja. Pia kula mbegu 10 za papai asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja.

Zambarau

Kula zambarau 15 hadi 20 kila siku kwa muda mwezi mmoja au zaidi.

Mchunga

Kiganja kimoja cha chunga (majani na mmea), ongeza glasi moja na nusu ya maji chemsha kwa muda wa dakika 15, kunywa baada ya kupoa. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja.

Wakati unaendelea na matibabu haya, usile vyakula vyenye asili ya nyama, tumia sukari na vyakula vya wanga kidogo.

Msubili, chumvi
Chukua nusu futi ya kipande cha msubili, katakata vipande vidogo na chumvi kidogo, kisha kula. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku 14.

Nyanya na pilipili manga
Glasi moja ya juisi ya nyanya, ongeza chumvi kidogo na unga wa pilipili manga nusu kijiko cha chai, kunywa kila asubuhi. Tiba hii kwa ajili ya tatizo la ini na homa ya manjao. Endelea nayo kwa muda wa siku 14.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment