Tuesday, 6 March 2018

Fanya haya unapobaini una apendeksi

Mtaalam Abdallah Mandai ameshika chombo chenye matunda yanachoche protini mwilini kuondoa matatizo mbalimbali ya kiafya.


KWA kuwa ni vigumu kutambua ugonjwa wa apendiksi, ni vema kwenda hospitali kupimwa ili kupata uhakika kama unao kabla ya kuanza tiba.

Baadhi ya dalili zake ni mauamivu ya ghafla ya tumbo yakifuatiwa na kuvurugika tumbo, kuharisha na baadaye maumivu kuhamia upande wa chini wa kulia wa tumbo.

Dalili zingine ni homa, kutapika, kizunguzungu na kukosa hamu ya chakula. Hata hivyo ukitumia maziwa, methi, karoti, bitiruti na tango vinasaidia kuondokana na tatizo hilo.

Maziwa

Tumia maziwa yaliyoondolewa mafuta lita moja kila siku kama tiba ya apendiksi, baada ya siku 14 nenda hospitali ukapimwe kutathmini maendeleo ya tiba.

Methi

Kijiko kimoja cha chai chenye mbegu za methi, weka katika lita moja ya maji, chemsha polepole kwa muda wa nusu saa, badaye ichuje na baada ya kupoa, kunywa maji yote. Endelea na tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja.

Karoti, bitiruti na tango

Changanya mililita 100 za juisi ya tango, nyingine kiasi hicho ya karoti na ya bitiruti kama hiyo, kisha kunywa. Fanya tiba hii mara mbili kwa muda wa wiki mbili.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao makuu yetu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment