Friday, 9 March 2018

Fanya haya uondokane na harufu mbaya mdomoni


Mtaalam Abdallah Mandai
TATIZO la harufu mbaya mdomoni ni la  kawaida kwa baadhi ya watu.

Mara nyingi waathirika huwa hawajitambui iwapo wana tatizo hilo na hata marafi zao wa karibu huwa wanakosa ujasiri wa kuwaambia.

Chanzo kikubwa cha tatizo hilo ni kuoza mizizi ya meno na kutunga usaa, matatizo ya fizi, mashimo  ndani ya meno yanayotunza mabaki ya chakula, matatizo ya mfumo wa upumuaji wa hewa kama mapafu, pua na koo.

Pia matatizo katika mfumo wa uyeyushaji wa chakula na kufunga kuchoo mara kwa mara. Baadhi ya tiba za harufu mdomoni ni methi, asali, mdalasini, mapera, parachichi, juisi ya matunda na mboga.

Methi

Chai iliyotengenzwa kwa kutumia majani ya methi husaidia kuondoa mgandamano wa maozeo mbalimbali ndani ya mwili.

Kwa kunywa kikombe kimoja cha chai ya methi kila siku asubuhi, inasaidia kuondoa harufu ya mdomoni na ya mwili kwa ujumla.

Asali/mdalasini

Chukua kijiko kimoja cha mezani cha asali, changanya na kingine cha mdalasini, baada ya kuchanganyika vizuri, lamba kidogokidogo hadi iishe, tiba hii ifanyike kila asubuhi baada ya kifungua kinywa. Asali ina uwezo wa kuua bakteria ndani ya mdomo.

Mapera

Mapera mabichi yana dawa za kuua wadudu mdomoni. Kula pera moja bichi (ukubwa wa kati) kila asubuhi baada kifungua kinywa, husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni na kuponyesha fizi zinazotoa damu. Kama tunda hakuna, tafuna majani matatu ya mpera.

Parachichi

Tunda la parachichi lina uwezo wa kuondoa uozo wa chakula ndani ya utumbo ambao ni mojawapo ya sababu kubwa ya harufu mbaya mdomoni. Kula nusu parachichi kila siku asubuhi baada ya kifungua kinywa.

Juisi ya matunda mboga za majani

Mwenye tatizo la harufu mbaya mdomoni anahitaji kula kilicho na viini vinavyohitajika katika ugonjwa huo. Juisi ya matunda na mboga mbalimbali ni chanzo kizuri cha viini hivi.

Mgonjwa ahakikishe kila siku anapata juisi ya tunda (au anakula tunda lenyewe) au juisi ya mboga.

Hata hivyo, licha ya kutumia tiba tajwa hakikisha unapiga mswaki kutwa mara mbili, kwa maana ya asubuhi na jioni sanjari na kuondoa mabaki ya nyama ndani ya meno.

Mwone daktari kama meno yako yanahitaji marekebisho, mswaki wa muarobaini utakuongezea kinga zaidi ya meno.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment