Thursday, 29 March 2018

Hatari zilizojificha ndani ya bafu lako


Bafu la kisasa

WATAFITIi nchini Uingereza wanasema usafi wa bafuni ni jambo linalofaa kuzingatiwa kuliko wengi wanavyodhania.

Profesa John Oxford, katika chuo Kikuu cha Queen Mary cha London, ameiambia BBC kuwa: "Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu''
"Watu hutumia muda wao katika kusafisha vyoo vyao lakini ingelikuwa vema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia dawa za kuuwa bakteria.
Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini sana, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria.
Hatari nyingine kwa watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho (shower) ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kwenye kifaa hiki ambacho kinaweza kuwa moto sana na kuuchoma mwili.
Msemaji wa kituo cha utafiti Rospa ameiambia BBC: " Tunawaomba watu kuweka maji baridi kwanza ndani ya beseni/ vidimbwi vya maji ya kuoga kwa ajili ya watoto . Kwa kufanya hivyo unawaepusha watoto na hatari ya kuungua kwao wanapojaribu kujifungulia maji ya moto.
"Kuna uwezekano mkubwa kwamba pale unapoweka maji moto kwenye beseni/ama kidimbwi cha maji ya kuoga watoto wanaweza kuyanawa na kuungua, lakini unapoweka maji ya baridi kwanza ndani ya beseni na baadaye kuyachanganya na ya moto, uwezekano watoto kuungua utakuwa ni mdogo.
Kwa kawaida unapotumia kipande cha sabuni cha kuoga unatarajia kitasafisha mikono yako kwa hivyo si rahisi kufikiria kwamba kinaweza kuwa kitovu cha vimelea vya maambukizi.
Hata hivyo, unaweza kuwa unajidanganya, kulingana na wataalam wa masuala ya afya.
Profesa wa Oxford anasema: "Bakteria wanaweza kukaa kwenye sabuni ya kuogea na kuhama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine - mfano bakteria aina ya E.coli ambao huishi maeneo hayo.
" Ikiwa mtu atatoka nje ya kikundi cha familia akiwa na bakteria ama mmoja wa familia akipata bakteria hao , basi bafu litakuwa mahala salama kwa bakteria hao kuishi na kusambaa kwa familia nzima."
Profesa wa Oxford anashauri kuwa matumizi ya sabuni ya maji ni bora kuliko kipande cha sabuni kwa matumizi ya kifamilia .
Na taasisi ya kitaifa ya afya na ushauri bora wa kiafya nchini Uingereza iliwashauri maafisa wa afya nchini humo kutumia sabuni za maji ama zilizowekwa kwenye chupa kunawa mikono.
Taulo iliyokaushwa vizuri na pengine ukaipiga pasi , ni bora kwa kukausha mikono ama uso wako unapokuwa na maji nyakati za mchana.
Lakini usiruhusu kwa namna yoyote ile mtu mwingine aitumie, anashauri Profesa Oxford.
"Taulo ni kitu chenye utata," alisema Profesa Oxford. "Usiwahi kutumia kamwe taulo moja na mtu mwingine - Sishauri hilo."
Ni jambo la kawaida kwa watu kutumia taulo moja katika maeneo ya sinki za bafuni/chooni ambayo hutumiwa na wanafamilia na hata marafiki wanaotembelea familia.
Hata hivyo , Profesa Oxford anasema: "Ni heri kuepukika'' . Vimelea vya magonjwa /bakteria vinaweza kukaa kwenye taulo kwa saa nne. Kusema ukweli taulo ni mahala pazuli kwao kukaa kwa sababu hewa imefunikwa na kuwa nzito
"Ningeshauri karatasi laini zitumiwe kama kukausha mikono badala ya taulo na kutupwa kwenye debe la taka au kila mtu awe na taulo yake"
Utafiti kuhusu athari za kuingia katika bafu lako na vifaa vingine mfano doli za plastiki unapoenda kuwaogesha watoto wadogo kunaweza kusababisha hatari kubwa.
Gazeti la Times limeripoti juu ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uswiss ya Sayansi na Teknolojia ambapo watafiti walifanyia uchunguzi doli zinazochezewa na watoto wakati wa kuoga na kubaini kuwa asilimia 58 ya doli hizo zilikuwa na bakteria hatari aina ya fangasi.
Mkuu wa utafiti huo alionya watu wasiwarushie watoto wao maji usoni kwa kutumia doli za kuchezea kwani anasema inaweza kusababisha "maambukizi ya macho, maskio au hata ya tumbo".

Ni dhahiri kwamba kuanguka bafuni kuna madhara yake makubwa , sabuni na maji kwa pamoja huifanya sakafu kuwa ya kuteleza.
Watu hupata majeraha ya mara kwa mara kwa kuvunjika mifupa , majeraha ya mwili, na vidonda wanapoingia ama kutoka bafuni , ama wakati mwingine huanguka kwenye sakafu yenye unyevunyevu
Kujaribu kupunguza matatizo haya, watu wanashauriwa kutumia mazulia ya bafuni kwenye sakafu,mazulia ya kuzuwia kuteleza ndani ya vidimbwi vya maji na kusafisha mabomba na sakafu za bafu mara baada ya kulitumia.

1 comment: