Thursday, 1 March 2018

Hiki ndicho kitunguu kiboko ya tatizo la kukojoa mara kwa maraKATIKA hali ya kawaida kuna kipindi cha muda ambao mtu anaweza kwenda haja ndogo kuashiria aina yoyote ya matatizo hata kama amekunywa maji mengi.

Iwapo kwenda haja ndogo itakuwa ni katika vipindi vifupivifupi, basi kuna tatizo linalopashwa  kushughulikiwa.

Baadhi ya tiba ambazo zinaweza kujaribiwa katika kutibu tatizo hili ni pamoja na kitunguu maji, asali na zambarau.

Kitunguu maji na asali

Vijiko viwili vya mezani vya juisi ya kitunguu maji na kijiko kimoja cha mezani cha asali changanya pamoja na kunywa. Fanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 21.

Zambarau

Kausha kilo mbili za zambarau, saga ili kupata unga laini, chukua nusu kijiko cha unga wa zambarau katika nusu glasi ya maji ya uvuguvugu kunywa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya ikiwemo ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment