Saturday, 31 March 2018

Hizi ndizo zabibu kiboko ya ugonjwa wa fizi za menoUGONJWA wa fizi za meno huathiri ngozi nyembamba inayozunguka mizizi ya meno na kusababisha kutungwa usaa, kulegea meno, na kusinya fizi.

Ugonjwa huu ukiendelea unaweza kusababisha matatizo katika mfumo wa uyeyushaji chakula kwa sababu ya mlundikano wa uchafu tumboni,      unaotoka kwenye fizi za meno.

Chanzo kikuu cha ugonjwa huo ni kutosafisha meno mara kwa mara, hatua inayosababisha bakteria kuzaliana juu ya meno na kuanza kuleta madhara kwenye fizi.

Zipo tiba asili mbalimbali zinazosaidia mgonjwa wa ugonjwa huu kuondokana na tatizo hilo. Zabibu, limau, ndimu, machungwa, mapera, komamanga, letusi na mnanaa ni miongoni mwazo.

Zabibu

Tindikali iliyomo ndani ya zabibu ni dawa madhubuti kwa bakteria waliomo ndani ya mdomo. Tumia zabibu pekee kama chakula kwa muda wa siku saba na baadaye tumia robo kilo ya zabibu mara tatu kwa siku muda wa siku 21, wakati huo ukiendelea na vyakula vingine.

Limau, ndimu na machungwa

Matunda tajwa yote yana vitamin C kwa wingi ambayo ni muhimu katika uponyeshaji wa vidonda, majeraha ya aina mbalimbali. Kula matunda hayo kwa wingi kunasaidia kuponyesha tatizo la fizi.

Mapera

Tafuna pera moja bichi kila asubuhi au majani matatu ya mpera, pia unaweza kuchemsha mizizi ya mpera ndani ya maji,na kusukutua mdomo mara tatu kwa siku.

Komamanga

Chukua kijiko kimoja cha chai cha unga wa ganda la tunda la komamanga, ongeza nusu kijiko cha chai cha pilipili manga na kiasi kama hicho cha chumvi, changanya vizuri na nusu lita ya maji, sukutua mdomo kwa maji hayo mara tatu kwa siku, muda wa siku 14.

Letusi

Tafuna majani mawili ya letusi kila baada ya mlo kwa muda wa mwezi mmoja.

Mnanaa

Tafuna majani mawili ya mnanaa kila baada ya chakula kwa muda wa mwezi mmoja.

Hata hivyo, ni vema iwapo umekumbwa na tatizo hilo njoo kituoni kwetu kupata maelezo ya kina ya namna ya kutumia dawa tajwa.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment