Thursday, 29 March 2018

Huu ndiyo ulimi wa mama mkwe kiboko ya maumivu ya sikioMASIKIO ni miongoni mwa viungo muhimu katika miili ya wanyama akiwemo binadamu. Viungo hivi ndivyo vinavyomsaidia kuepukana na matatizo mengi ikiwemo vifo.

Masikio yanamsaidia mwanadamu kusikia kishindo cha adui na hivyo kujihami, pia ndiyo yanamfanya awe makini anapofanya mambo mbalimbali yanamwezesha kuishi.

Kutokana na umuhimu huo wa masikio, inapotokea yanamuuma anakuwa katika wakati mgumu na hivyo kulazimika kutafuta haraka dawa ya kumponya.

Zipo aina nyingi za tiba asili ambazo zinaweza kumsaidia aondokane na tatizo hilo, miongoni mwazo ni ulimi wa mama mkwe, tangawizi, kitunguu swaumu, nachufwo na nyonga mbembe.

Ulimi wa mama mkwe

Kipande kidogo cha jani la ulimi wa mama mkwe, kiponde kisha kamulia tone moja mara mbili kutwa kwa muda wa siku tatu. Weka pia kipande cha jani hilo sikioni hadi maumivu yaishe.

Tangawizi

Kamulia juisi ya tangawizi sikioni kutwa mara mbili baada ya kuiponda. Itumie kwa muda wa siku tatu.

Kitunguu swaumu

Punje moja ya kitunguu swaumu iponde kisha weka matone ya maji kupata unyevu, kamulia matone mawili katika sikio linalouma mara mbili kutwa, kwa muda wa siku tatu.

Nachufwo

Kamulia sikioni mara mbili kutwa majani ya nachufwo yalipondwa na kuchangaywa na maji kidogo, fanya hivyo kwa muda wa siku tatu.

Nyonga mbembe

Kamulia sikioni mara mbili kutwa majani ya nachufwo yalipondwa na kuchanganywa na maji kidogo, fanya hivyo kwa muda wa siku tatu.

Ni vema iwapo unapopatwa na maumivu ya masikio ukaja kituoni kupata maelezo ya kina kuhusu matumizi sahihi ya dawa hizi ili kupata matokeo bora.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

1 comment:

  1. What do this plant tongue of"mother-in-law" especially do or treat?
    Dr.Mike

    ReplyDelete