Sunday, 4 March 2018

Ijue nguvu ya kitunguu swaumu kwa maradhi ya moyo


kitunguu swaumu

MAGONJWA ya moyo yamo miongoni mwa maradhi yasiyoambukiza ambapo mgonjwa anapaswa kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya.

Hata hivyo, pamoja na tiba zinazopatikana hospitali, maradhi hayo pia yanatibiwa kwa kutumia asparagasi, kitunguu swaumu, kitunguu maji na tende.

Kitunguu swaumu

Wataalamu wa tiba asilia wamethibitisha kwamba kitunguu swaumu kinazuia tatizo la kuuma kwa moyo na kurekebisha kiherehere cha moyo.

Pia hupunguza kolestero iliyo katika mishipa ya damu. Tumia punje tatu za kitunguu swaumu kila siku jioni kwa muda wa mwezi mmoja.

Asparagasi (namna ya boga)
Ili kutibu moyo dhaifu au uliopanuka, tengeneza juisi ya asparagasi iliyochumwa siku hiyohiyo vijiko vitatu vya chai.

Changanya na asali vijiko viwili vya chai, tumia kijiko kimoja cha mchanganyiko huo mara tatu kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja. Baada ya muda huo nenda hospitali kupimwa ili kutathmini maendeleo ya tiba.

Kitunguu maji

Ili kurekebisha matatizo ya moyo, tumia gramu 100 za kitunguu maji (cheupe) kila siku. Unaweza kutengeneza kachumbari ya kitunguu maji na kuongeza mbogamboga nyingine.  Endelea na tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja.

Tende

Chukua robo kilo ya tende, loweka ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mzima, asubuhi yake fikicha ndani ya maji hayo. Kunywa maji yote na kiini cha tende. Tiba hii ifanyike mara tatu kwa siku kwa muda wa miezi minne hii ni tiba kwa ajili ya moyo ulio dhaifu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo au ushauri wa kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment