Monday, 12 March 2018

Ijue nguvu ya pera kwa maradhi ya kiherehere cha moyo


Pera

KIHEREHERE cha moyo ni ugonjwa ambao mapigo ya moyo wa mgonjwa huenda mbio au kupishana bila mpangilio. Kimsingi ni rahisi mgonjwa kugundua kwamba analo tatizo hilo.

Chanzo cha kiherehere cha moyo ni moyo kufanya kazi ya ziada kusukuma damu, wasiwasi, uvutataji sigara na kufunga choo.
Tunda la mpera, asali na zabibu ni miongoni mwa tiba za tatizo hili.

Tunda la mpera (pera)

Kula pera moja kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote kwa muda wa mwezi mmoja, tiba hii ni kwa ajili ya kiherehere cha moyo kilichosababishwa na wasiwasi au upungufu wa damu.

Asali

Chukua glasi moja ya maji, ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asali, kamulia nusu limau ndani ya maji hayo, changanya vizuri na kunywa kabla ya kwenda kula kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.

Zabibu

Kunywa glasi moja ya juisi ya zabibu mara mbili kwa siku muda wa mwezi mmoja.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia virutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment