Monday, 5 March 2018

JK asaidia mifuko 300 ya saruji Kwakonje


Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (kulia), akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msada wa saruji. Katikati ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na kushoto ni mkewe Salama Kikwete.

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete, ametoa mchango wa mifuko 300 ya saruji itakayofanikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kwakonje na nyumba za walimu.

Msaada huo ameukabidhi kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (CCM), akishuhudiwa na mbunge wa kuteuliwa Salma Kikwete ambaye ni mkewe na wananchi wengine wa eneo hilo.

Kikwete ambaye pia mbunge wa zamani wa jimbo hilo, ametoa msaada huo ili kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho kuondokana na changamoto ya kufuata umbali mrefu huduma za afya.


No comments:

Post a Comment