Thursday, 15 March 2018

Kabili tatizo la jongo kwa kufanya moja ya mambo hayaMtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

JONGO ni ugonjwa unaowapata zaidi wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 35 na wanawake waliokoma hedhi. Shambulio la jongo linaambatana na maumivu makali ya ndani ya dole gumba mguuni, joto kali na uvimbe.

Ugonjwa huu pia unaweza kushambulia kifundo cha mguu, kiungo cha goti, kiwiko cha mkono na viungio vya mwili (joints) vingine.

Chanzo kikubwa cha maumivu hayo ni chembe ndogo za tindikali inayoitwa yuriki asidi ndani ya viungo tajwa, figo na ngozi ya mwili.

Kunapokuwa na asidi ya yuriki nyingi mwilini kuliko ile inayohitajika hutengeneza chembechembe kama sindano katika sehemu ya viungo tajwa na kusababisha maumivu makali.

Unaweza kupata maradhi haya iwapo unakula kiasi kikubwa cha vyakula vya protini na kabohaidreti, kutofanya mazoezi ya kutosha, kutumia pombe na kutokunywa maji ya kutosha.

Kabla ya kuanza kutumia tiba hakikisha unafanya mabadiliko katika vyakula, vinywaji na vyote ambavyo sababu ya kuwa na maradhi haya.

Miongoni mwa dawa unazoweza kutumia kutibu maradhi hayo ni pamoja na kufunga, nyonyo, tofaa, ndimu na ndizi.

Kufunga
Iwapo tatizo la ugonjwa ni kubwa zaidi anza kufunga chakula na badala yake kunywa juisi ya chungwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Nyonyo
Ponda mbegu za nyonyo hadi ziwe laini kisha paka sehemu zilizoathirika, fanya hivyo mara tatu kwa siku muda wa siku saba.

Tofaa

Maliki asidi ambayo ni tindikali ndani ya tofaa ina uwezo wa kukomesha yuriki asidi ya ziada ndani ya mzunguko wa damu. Kula tofaa moja kila baada ya mlo kwa muda wa siku saba.

Ndimu

Sitiriki asidi ndani ya ndimu ina uwezo wa kukomesha yuriki asidi ya ziada katika mzungumko wa damu, hivyo kuifanya ndimu kuwa tiba ya jongo.
Tumia juisi ya ndimu  moja ndani ya glasi moja ya maji asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Ndizi

Kwa muda wa siku nne tumia ndizi za kupikwa pekee, katika milo yako yote. Usitumie zaidi ya ndizi 10 kwa siku.

Fanya tiba mojawapo ya hizo kwa muda wa siku tatu, funga tena kwa kutumia machungwa pekee kwa muda wa siku tatu, malizia tiba kwa muda wa siku zinazofuata.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment