Tuesday, 27 March 2018


Kamati ya Bunge ya Bajeti inavyoendelea na vikao vyake mjini Dodoma

 Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Maria Kangoye akizungumza wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo Riziki Lulidi.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo kwenye picha) wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutokaWizara ya Fedha na Mipango walioongozwa na wake Dk. Philip Mpangowakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019, katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma.



Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Albert Ntabaliba akizungumza wakati wa kupitia na kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika jana ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.


ACT, CUF waunga mkono waraka wa Maaskofu KKKT


Nuru Athumani

CHAMA cha Wananchi (CUF) na ACT-Wazalendo wameunga mkono waraka maalum wa Pasaka uliotolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), na kuitaka serikali kufanyia kazi hoja zilizomo kwenye waraka huo.

Akizungumza na wanahabari jana Dar es Salaam Katibu Mkuu CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema anaunga mkono waraka huo kwa kuwa maaskofu hao wametekeleza wajibu wao wa kusemea waumini wanaowaongoza.

“Mimi binafsi nafarijika pale ambapo taasisi za kidini zinaposimama wanapoona mambo hayaendi sawa. Sio lengo lao kuikosoa serikali bali kuweka mambo sawa, msiwatafsiri kama wameingia kwenye siasa. Ni wajibu wao kuwasemea waumini,” amesema Maalim Seif. 

Naye Mratibu wa Itikadi Mawasiliano na Uenezi wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo Karama Kaila amesema ngome hiyo inaunga mkono waraka huo na kuitaka serikali kuyafanyia kazi malalamiko yaliyomo na kupuuza watu wanaosema kuwa viongozi wa dini wako kisiasa. 

“Ngome ya vijana inawapongeza sana kwa kutekeleza wajibu wao, ushauri wa maaskofu na maoni yao inabidi kuchukuliwa uzito wa hali ya juu, wamezungumzia kuhusu uhuru wa kutoa maoni, mauaji ya watu, katiba mpya, uchumi na ajira kwa vijana, ni mambo muhimu kwa watanzania wote bila kujali tofauti zetu kuyaunga mkono.

“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema viongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao,” amesema.


Rais Dk. John Magufuli akizindua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dar es Salaam jana (Machi 26,2018).



Rais Dk. John Magufuli akikagua ghala la dawa kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018). Pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Linden Morrison na viongozi wengine.



Sehemu ya magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), yaliyozinduliwa  Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018). 




Rais Dk. John Magufuli akimshukuru Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund, Linden Morrison wakati akijaribu moja ya magari  181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), aliyozindua Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).


Rais Dk. John Magufuli akikagua sehemu ya magari  181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD),  aliyozindua Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund, Linden Morrison na viongozi wengine.


 Rais Dk. John Magufuli akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).




Sehemu ya wafanyakazi wa MSD wakimshangilia Rais Dk. John Magufuli  wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).



Rais Dk. John Magufuli akikata utepe kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund, Linden Morrison na viongozi wengine.

Rais Dk. John Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund  Linden Morrison akijaribu moja ya magari  181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) aliyozindua Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).


Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakipiga picha msafara wa Rais Dk. John Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund,Linden Morrison  (kushoto) na viongozi wengine wakati wakielekea kukagua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa(MSD), aliyozindua Dar es Salaam jana (Machi 26, 2018).

No comments:

Post a Comment