Friday, 2 March 2018

Kenya yawasimamisha kazi madaktari waliompasua mgonjwa asiyestahili


Hospitali ya taifa ya Kenyatta

MADAKTARI katika Hospitali ya Kenyatta, wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.

Taarifa kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, zinabainisha kuwa wagonjwa wawili waliokuwa hawajitambui na mmoja kati yao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu iliyoonekana imeviria.

Lakini pia mkurugenzi huyo ameomba radhi na kusema "tunafurahi kuwatangazia umma kwamba mgonjwa huyo sasa ametibiwa na anaendelea vizuri"

Wafanyakazi wanaochunguzwa katika sakata hilo ni pamoja na daktari wa upusuaji wa ubongo, muuguzi na mtalaam wa dawa za usingizi.


No comments:

Post a Comment