Saturday, 31 March 2018

Kusainiwa muhtasari wa upimaji mpaka baina ya Tanzania na Kenya


Kiongozi wa Ujumbe wa wataalam wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania, Huruma Lugala akibadilishana muhtasari  na Mkuu wa Taasisi ya Usimamizi wa Mipaka  Kimataifa wa Kenya (KIBO) Bibi Justor Nkoroi mara baada ya kila mmoja kusaini kwa niaba ya Serikali ya nchi zao.

Muhtasari huo uliosainiwa wilayani Tarime mkoani Mara hivi karibuni ndio  muongozo unaotumika katika kazi ya kuimarisha mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya kwa wataalam wa nchi zote mbili kwa kipande cha mpaka wa urefu wa Kilomita 238 kuanzia Kando ya Ziwa Victoria (mkoani Mara) Hadi Ziwa Natron mkoani Arusha.  (PICHA NA REHEMA ISANGO, WANMM)

No comments:

Post a Comment