Tuesday, 6 March 2018

Kuzuia GMO hakuna faida kwa mkulima- Prof. Maghembe
Prof. Jumanne Maghembe

Suleiman Kasei

MBUNGE wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe amesema hatua ya Tanzania  kuweka Sheria  na kanuni ngumu ili kuzuia uzalishaji wa mazao yatokanayo na Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO), huku wananchi wake wakiwa watumiaji wakubwa wa bidhaa za teknolojia hiyo haina faida kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na mwandishi wetu ambapo amesema kukosekana kwa uamuzi wa haraka katika kutumia GMO kunarudisha nyuma jitihada za wakulima.
 Mbunge huyo ambaye awali alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema katika zao la pamba ambalo linalimwa bila kutumia GMO huku nguo zinazovaliwa nchini asilimia 75 zikiwa zimetokana na pamba ya teknolojia hiyo.

Alisema ni swali la kujiuliza kama nchi ni kwanini nchi kama Marekani, Urusi, China, India, Pakistan, Misri,  Sudan, Mali, Bukina Faso na Kenya zimeamua kuzalisha Pamba yake kwa GMO na kuachana na ile ya kienyeji.

Maghembe alisemaa pamba ya teknolojia haina madhara inapolimwa, kuvunwa, kutengenezwa kuwa bidhaa na katika kutumia bidhaa zake. “Mpaka leo sijaona matokeo ya tafiti za kisayansi inayoonesha madhara,” amesema.

No comments:

Post a Comment