Tuesday, 6 March 2018

Lissu: Uchaguzi wa marudia haukuwa huru na wa haki

Suleiman Kasei


MBUNGE wa Sindiga Mashariki, Tundu Lissu amesema taarifa iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuhusu chaguzi za marudio ni uthibitisho mwingine kwamba hakukuwa na uchaguzi bali ni uhuni wa kisiasa tu.

Lissu amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari hizi aliyetaka kufahamu  amepokeaje taarifa ya LHRC kuhusu uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni na Siha. 

Amesema kituo hicho kimekuwa kikionesha madhaifu makubwa kutokana na usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), katika chaguzi mbalimbali jambo ambalo wahusika hawapendi kusikia.

Amebainisha kuwa kitendo cha NEC kutokubaliana na taarifa hiyo hakina mashiko kwani hata Rais Dk. John Magufuli alishawaagiza wakurugenzi wa halmashauri za serikali za mitaa kutokuwatangaza wapinzani pale wanaposhinda chaguzi. 

No comments:

Post a Comment