Thursday, 29 March 2018

Lowassa, Sumaye waondoka mahakamani kwenda kumzika KimeseraMAWAZIRI wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa wameondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya muasisi wa Chadema, Victor Kimesera.

Viongozi hao walifika mahakamani hapo leo asubuhi Machi 29, 2018 kusikiliza kesi inayowakabili viongozi sita wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Kimesera alifariki dunia Machi 24, 2018 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni.

No comments:

Post a Comment