Friday, 16 March 2018

Mafuriko yaikumba Kenya


BAADHI ya maeneo nchini Kenya yameathirika vibaya baada ya mafuriko ya ghafla kukata mawasliano ya barabara. Ripoti kutoka maeneo mbalimbali nchini humo zinasema nguvu ya maji ilikuwa kubwa hivyo baadhi ya watu na magari kusukumwa.
Shirika la Msalaba Mwekundu limeripoti kuwa watu watano waliokuwa kwenye lori walisukumwa na maji eneo la Kitui kilomita 180 Mashariki mwa Nairobi.
Shirika la Msalaba Mwekundu kwenye ukurasa wake wa Twitter limesema baadhi ya barabara nchini humo zimeharibiwa ikiwemo barabara ya Kajiado-Namanga Kusini mwa Kenya na kufanya eneo hilo kushindwa kupitika.
Maelfu ya wakazi wa Nairobi wamekwama na kushindwa kuendelea na shughuli zao kwa sababu ya mvua hizo.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo miundo mbinu ya barabara za miji ya Nairobi haziwezi kumudu.

Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Nairobi yalikwama huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.
Kawaida msimu wa mvua nchini Kenya huwa kati ya mwezi Machi na Mei, lakini wadadisi wanasema safari hii mvua imenyesha kwa wingi zaidi.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment