Wednesday, 28 March 2018

Mahakama Kenya yaagiza Miguna aachiliweMiguna Miguna wa pili kulia mwenye kofia, akiwa na wanasheria wake katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta alipozuiwa kuingia Kenya kabla ya mahakama kuagiza aachiliwe
JAJI wa mahakama kuu, nchini Kenya, Roseline Aburili ameagiza wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna kuachiliwa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Miguna ameagizwa kwenda mahakamani leo Jumatano sasa 3:00 asubuhi  hii kwa saa za hapa Afrika Mashariki.
Miguna alirejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada majuma sita yaliyopita.
Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea nyumbani. Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.
Maofisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya
shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

No comments:

Post a Comment