Thursday, 29 March 2018

Mahakama yaruhusu Habinder Sethi kwenda hospitali kupatiwa matibabu
MMILIKI wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi ameruhusiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa kudai anaumwa na hivyo anahitaji kupata matibabu.

Aidha, Wakili wa Serikali Leonard Swai aliiomba mahakama ifuate taratibu za magereza, hata hivyo alidai ni kweli mshtakiwa hali yake kiafya ni dhaifu.

Katika hatua nyingine, Wakili wa Takukuru, Pendo Temu alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba wanafanya mawasiliano nje ya nchi ya kupata nyaraka muhimu katika kukamilisha upelelezi. Pia ameomba kuchukua maelezo ya mshtakiwa pindi afya yake itakapoimarika.

No comments:

Post a Comment