Friday, 2 March 2018

Majimaji ya mgomba kiboko kwa tiba ya bawasili


 Migomba ambayo unaweza kupata ganda kwa ajili ya matibabu ya kikundu au bawasili

KIKUNDU au bawasili ni ugonjwa unatokea baada ya kuathiriwa kwa mishipa ya damu ndani au nje ya njia nya haja kubwa.

Wakati mwingine mishipa inaweza kupasuka na kuteleza kisha kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa.

Ugonjwa huu unasababishwa na  kufunga choo, kusimama au kukaa kwa muda mrefu, kazi ya kutumia nguvu, udhaifu wa misuri ya mwili na unene kupita kiasi.

Kutokana na mimea tiba na matunda unaweza kutibu ugonjwa huu ambao mtu wa rika na jinsia yoyote unaweza kumpata.

Tiba hizo ni pamoja ni kupaka majimaji ya mgomba, kutumia mbegu za embe,  za ufuta, karea, komamanga, radishi nyeupe, kitunguu maji, muarobaini na majani ya mbalika.

Maji ya mgomba

Chukua majimaji ya ganda la mgomba, paka kwenye kikundu wakati wa asubuhi, mchana na jioni. Tiba hii iendelezwe kwa muda wa siku saba.

Majani ya mbalika

Chukua nusu kilo ya majani ya mbalika. Chemsha kwa muda wa dakika 15 katika maji yenye ujazo wa lita mbili, kunywa glasi moja mara tatu ya maji hayo kwa siku, kwa muda wa siku saba. Tiba hii inasaidia kurudisha mgongo uliotoka nje.
Mbegu za embe

Kausha mbegu za embe kwenye kivuli, saga kutengeneza unga laini, chukua nusu kijiko cha chai cha unga wa embe, weka ndani ya maji nusu glasi, ongeza asali kijiko kimoja cha chai, koroga na kunywa. Tiba hii ifanyike asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Mbegu za ufuta

Chukua vijiko sita vya mezani vilivyojaa ufuta, weka ndani ya maji lita moja na nusu, yachemshe hadi yataakapo baki lita moja, baada ya kupoa chuja na yatunze kwenye chombo kisafi. Tumia nusu glasi mchana na jioni kwa muda wa siku saba.

Karea

Chukua mizizi ya karea iliyosafishwa ipasavyo, ponda na weka katika njia ya hajakubwa, baada ya saa moja ondoa, fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Au tengeneza juisi ya karea tatu chuja na changanya na glasi moja ya maziwa ambayo yameondolewa natuta, kunywa yote asubuhi. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku saba.

Komamanga

Kaanga fanda la komamanga bila mafuta hadi litakapokauka na kuwa jeusi, saga ili kupata majivu laini, changanya na mafuta ya karanga au pamba, weka katika njia ya haja kubwa mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 10.


Radishi nyeupe

Pondaponda radishi iwe laini, ongeza maziwa kidogo changanya vizuri, chukua kijiko cha chai cha mchanganyiko huo, weka katika njia ya haja kubwa. Fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.

Kitunguu maji

Chukua kitunguu kimoja chenye ukubwa wa kadri, tengeneza juisi yake katika nusu glasi ya maji, ongeza vijiko vya mezani sita vya sukari, koroga na kunywa, fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 10.

Muarobaini

Chukua kijiko kimoja cha chai cha unga wa ganda la ndani la muarobaini changanya na kijiko kimoja cha chai cha sukari guru. Weka ndani ya nusu glasi ya maji ya uvuguvugu. Changanya vizuri na kisha kunywa.

Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 10. Licha ya tiba hiyo, meza mbegu nne zilizowiva za muarobaini kila siku.
No comments:

Post a Comment