Friday, 9 March 2018

Mama Janeth apongeza jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchum Mama Janeth Magufuli
MKE wa Rais, Mama Janeth Magufuli ameupongeza mkoa wa Dar kwa kuanzisha vikundi zaidi 400 vya ujasiriamali vinavyolenga kumkomboa mwanamke.
Mama Janeth ametoa kauli hiyo wakati akihutubia maelefu ya wanawake katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni kilele cha siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa zilifanyika mkoani Tabora ambako mke wa Rais mstaafu Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Katika hotuba hiyo, Mama Janeth ameziomba asasi za kiraia na watu binafsi kushirikiana na Serikali kuwapa wanawake mbinu, mitaji, masoko na mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yatakayosaidia kuwakwamua kiuchumi.
Kila Machi 8 ya kila mwaka, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
Kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka 2018 ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini. Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati madhubuti yenye kumwezesha mwanamke kiuchumi.

No comments:

Post a Comment