Tuesday, 20 March 2018

Mama Samia ataka wananchi Pemba washirikiane


Mama Samia Suluhu Hassan.

Peter Simon, Pemba

MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha afya cha huduma ya mama na mtoto, Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kituo hicho kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo wananchi 5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto chini ya umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe na ustawi wa mama na mtoto.

Vijiji vitakavyofaidika na huduma ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani na Bule.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhimiza shughuli za maendeleo, Makamu wa Rais amekagua ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea muasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mrashi ambapo amemkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake inayojengwa na wanachama wa chama hicho eneo la Sizini.

Pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo amewataka kinamama kuwa mstari wa mbele kuonesha njia ya kuwa viongozi bora.


No comments:

Post a Comment