Saturday, 10 March 2018

Mamia wamzika Kabourou

Rhoda Ezekiel, Kigoma 

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu, Emanuel Maganga amewaongoza mamia ya wananchi na viongozi  wa vyama vya siasa wa serikali na katika mazishi ya mwanasiasa mkongwe nchini na Mwenyekiti msaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Kigoma, Dk. Amani
Kabourou.

Akizungumza katika msiba huo Brigedia Jenerali Maganga amesema Kaburu ni mwanasiasa aliyejikita kutetea haki za wananchi wa Kigoma na alikuwa wa kwanza kupigania maendeleo ya mkoa huo. Mwili wa Dk.
Kabourou umeshapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Amesema Serikali na CCM itamkumbuka Dk.
Kabourou kwa mchango mkubwa ambao ameufanya katika mkoa huo na amekuwa mfan o wa kuigwa na wengine.

"Marehemu  
Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake na alipokuwa kiongozi wa vyama mbalimbali na hata katika Bunge la Afrika Mashariki.
Hakika ameondoka lakini wana Kigoma tutamkumbuka daima na kwa wanasiasa wengi wanafahamu kuwa vijana wengi mkoani hapa wamejifunza siasa kutoka kwake," amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Amandusi Nzamba amesema CCM imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama kufikia malengo yake.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kama mtoto na mwanafunzi wa
Kabourou pamoja na tofauti za kisiasa ndiye aliyekuwa mwalimu wao na aliwazibua masikio wanasiasa wengi wa mkoa huo.

"Kaburu enzi za uhai wake ametufundisha wengi na hasa kuhusu siasa za Tanzania na kubwa zaidi alihimiza umoja na mshikamano mbele ya maendeleo ya Kigoma.Huyu ni kiongozi wa kwanza kupitia mfumo wa vyama vingi na ndiye mwalimu wetu katika siasa za vyama vingi.Alijitoa na kupambana na kupigania siasa za mkoa wetu wa Kigoma na amefanya kazi kubwa," amesema Zitto.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kigoma, Salim Kangeta amesema Dk.
Kabourou alikuwa ni kiongozi aliyeshirikiana na kila mtu na hata viongozi wa dini na kubwa zaidi alikuwa anasikiliza ushauri ili mkoa wa Kigoma usonge mbele kimaendeleo.


HISTORIA YA KABURU

Kaburu alizaliwa mwaka 1949 mkoani Kigoma na alisoma elimu yake ya msingi shule ya msingi Kipampa na elimu ya sekondari katika sekondari ya Living Stone, Kigoma.

Baada ya hapo aliondoka na kwenda kuendelea na masomo yake nchini Marekani ambapo baada ya hapo alirejea nchini na kuanza harakati za siasa.
Alikuwa mbunge wa Jimbo la Kigoma kwa kipindi cha miaka tisa, pia amewahi kuwa mbunge Bunge la Afrika Mashariki , Katibu Mkuu wa Chadema na amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma.

No comments:

Post a Comment