Monday, 5 March 2018

Manowari ya Marekani yatia nanga Vietnam

   Manowari hiyo inayotumia nishati ya nyuklia itatia nanga katika bandari wa Danang                 

MANOWARI ya Marekani Carl Vinson inafanya ziara ya kihistoria nchini Vietnam kwa mara ya kwanza kwa meli ya aina hiyo kuzuru Vietnam tangu vita kumazilika.
Manowari hiyo inayotumia nishati ya nyuklia itatia nanga katika bandari wa Danang ambapo wanajeshi wa Marekai walitua kwanza wakati wa vita. Hii ina maana ya kuonesha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo.
Lakini wadadisi wanasema hii inatuma ujumbe kwa China wakati inaendelea kujiimarisha maeneo ya kusini mwa bahari ya China. China kwa sasa ndio taifa lenye nguvu zaidi eneo hilo na pia mshirika mkubwa wa kibishara wa Vietnam.
Kwa hiyo utawala wa komunisti wa vietnam unachukua tahadhari kuzuia hatua ambazo zinaweza kuvuruga uhusiano na jirani yake China.
China inadai kumiliki karibu eneo lote la bahari ya Kusini mwa China vikiwemo visiwa ambavyo pia vinadaiwa na mataifa mengine.
Mara kwa mara Marekani imesema kuwa haiegemei upande wowote kwenye mzozo wa kusini mwa bahari ya China lakini jeshi la wanamaji wa Marekani limekuwa likiendesha doria eneo hilo ishara ya kuonesha ubabe wa kijeshi dhidi ya China.
Manowari ya USS Carl Vinsion imefanya safari nyingi kwenye eneo hilo wakati wa miongo kadhaa ya huduma zake na mara ya mwisho ilikuwa eneo hilo ilikuwa siku chache zilizopita.
Vita vya Vietnam ambavyo nchi hiyo huviita Vita ya Mareknia, vilikuwa vibaya. Serikali ya Vietnam inakadiria kuwa mamilioni ya watu raia na wapiganaji wa Komunisti waliuawa. Zaidi ya wanajeshi 58,000 wa Marekani nao waliuawa au kutoweka.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment