Friday, 23 March 2018

Masoko mapya kufunguliwa Tabata na Mbezi


Isaya Mwita


MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema halmashauri ya jiji hilo  inatarajia kufungua masoko mawili katika maeneo ya Tabata na Mbezi ili kuongeza mapato.

Amesema ukusanyaji kodi katika jiji hilo unakwenda vizuri na kwamba hadi sasa wamekusanya asilimia 54.

Mwita ametoa kauli hiyo leo baada ya kumaliza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa jiji hilo.

“Katika ukusanyaji kodi tunakwenda vizuri, hadi sasa tumeshakusanya asilimia 54, hadi kufika mwezi Julai tutakuwa tumevuka lengo,” amesema.

Kuhusu maendeleo ya masoko yanayomilikiwa na jiji la Dar es Salaam, ikiwemo la Machinga Complex na Kariako DDC, Meya Mwita amesema
kwa sasa yanaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment