Tuesday, 13 March 2018

Maziwa ya binadamu tiba nzuri ya sikio linalotoa usaaSIKIO kutoa usaa ni maradhi ambayo hayajaenea kwa wingi sana ila yamekuwa kero kubwa kwa wale waliothirika nayo.

Zipo tiba nyingi asili ambazo zimetoa mafanikio kwa wagonjwa  wa maradhi hayo yakiwemo maziwa ya binadamu.

Maziwa ya binadamu

Maziwa ya binadamu ni tiba nzuri kwa sikio linalotoa usaa. Weka matone manne ya maziwa ya mama katika sikio linalotoa usaa. Fanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa wiki moja.

Kitunguu

Kaanga punje sita za kitunguu swaumu katika milimita 100 za mafuta hadi yanapogeuka kuwa rangi ya kahawia na punje zote kuungua, chuja mafuta hayo na kuyaweka mahali safi na salama. Weka matone matatu ya mafuta hayo katika sikio, mara mbili kwa muda wa siku saba.

Kitunguu maji

Juisi ya kitunguu maji, ipashe moto hadi kukaribia kuchemka, wakati ikiwa vuguvugu, chukua matone matatu hadi matano, weka ndani ya sikio mara mbili kwa siku muda wa siku saba. Wakati wowote kabla ya kuweka juisi hiyo sikioni hakikisha unaipasha moto kidogo.

Muarobaini

Tengeneza juisi ya majani ya muarobaini, changanya kiasi kinacholingana nayo cha asali, pasha moto mchanganyiko huo, chukua matone matatu weka ndani ya sikio mara tatu kwa muda wa siku saba. Hii pia ni tiba ya jipu ndani ya sikio.

Ndimu

Juisi ya ndimu yenye ujazo wa milimita 100 hadi 200 bila kuchanganya na kitu kingine, weka ndani ya chupa safi yenye rangi nyeusi acha juani kwa muda wa siku tano, ili kutibu sikio linalotoa usaa, weka matone matatu ya juisi hii mara tatu kwa muda wa siku saba.

Mpungate

Jani la mpungate lipashe moto hadi lishike moto, kamua maji katika jani hilo, weka matone matatu ya jani hayo katika sikio kwa muda wa siku saba.

Tangawizi

Tengeneza juisi ya tangawizi mbichi inayotosha vijiko vitatu au vinne vya mezani, ongeza chumvi ya mawe kidogo, chuja na kutunza chupa iliyojaa, Tumia matone matatu katika sikio mara mbili muda wa siku saba.

Mgagani

Osha majani ya mgagani kwa maji moto, ponda na kukamulia ndani ya sikio matone matatu kwa siku. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku saba.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment