Wednesday, 7 March 2018

Mbunge mstaafu afariki duniaMarehemu Dk. Amani Kabourou

ALIYEWAHI kuwa mbunge wa Kigoma Mjini, Dk. Amani Kabourou amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.

Dk. Kabourou ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amefariki akiwa na umri wa miaka 79, alizaliwa mwaka 1949.

Wakati wa uhai wake licha ya kuwa mbunge wa Jamhuri, pia alikuwa mbunge wa Bunge la Afrika Masharikia, kati ya mwaka 2007 hadi 2012 pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Kigoma baada ya kuhama Chadema.

Mbunge wa sasa wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema kupitia ukurasa wake wa facebook kuwa huo ni msiba mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment