Tuesday, 13 March 2018

Mbunge Uganda aunga mkono wanawake kupigwa na waume zaoTwinamasiko Onesimus
MBUNGE wa Uganda, Twinamasiko Onesimus mewaacha watu na butwaa baada ya matamshi yake yaliyoonekana kuunga mkono wanawake kupigwa na waume zao.
Onesmus Mbunge wa jimbo la Bugangaizi Mashariki, amesema maneno hayo yakushangaza akiwa katika mahojiano na kituo cha televisheni cha NTV Uganda.
“Kama mwanaume lazima umuadhibu mke wako mguse kidogo, mkamate na umnyooshe vizuri,”amesema.

Kipande hicho cha video kilisambazwa na mwandishi wa NTV kwenye mtandao wa Twitter na watu hawakusita kutoa maoni kwa haraka.

Bala Davis anauliza ' je na mwanamke pia anafaa kumchapa mwanaume?'
Issa Kato ameuliza je, huyu hajakiuka taratibu za kibunge?
Inaonekana Onesimus aliyeoa alikuwa anajibu tamko alilolitoa Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwenye siku ya wanawake , aliposema wanaume wanaowapiga wake au wapenzi wao ni waoga.
“Wanaume wanaowapiga wanawake ni wapumbavu na waoga aliwaambia watu katika sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Kikristo cha Uganda.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor , zaidi ya moja kati ya wanawake watano wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamepitia unyanyasaji wa majumbani na kingono nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment