Monday, 12 March 2018

Mhifadhi wanyamapori asimamishwa kaziDk. Hamisi Kigwangala

Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala amemsimamisha kazi, mhifadhi Wanyapori mkuu, Emanuel Barabara ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kushirikiana na majangili kuhujumu rasilimali za misitu nchini.

Barabara ambaye pia Mkuu wa kanda Pori la Akiba Rukwa, lililopo wilayani  Mlele, mkoa wa Katavi, Dk. Kingwangala amesema amemsimamisha tangu Machi 10 mwaka huu.

Sanjari na hilo, Dk. Kingwala ameagiza kuundwa kamati ya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo na iwapo itabainika amefanya kosa hilo, hatua kali za kinidhamu dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni.

“Tunatoa onyo kali kwa watumishi wa wizara wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa rasilimali za misitu, wanyamapori na malikale kuacha mara moja kwani hatutasita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo ikiwemo kufukuzwa kazi,” amesema Dk. Kigwangala.

Ametoa mwito kwa watumishi wa wizara yake, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya uhifadhi rasilimali za nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

No comments:

Post a Comment