Thursday, 1 March 2018

Mkojo wa ng’ombe mwenye mimba kiboko ya kifaduro


 Watu wakinywa mkojo wa ng'ombe wakiamini kuwa ni kinga na tiba ya maradhi mengi

KIFADURO ni kikohozi kinachowashika watoto wadogo wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na mitano. Kwa nadra watoto wenye umri zaidi ya huo wanaweza kuugua ugonjwa huo.

Kifaduro kinasababishwa na vijidudu wanaoitwa kwa lugha ya kitaalamu ‘bordetella pertussis’ na ni ugonjwa unaoambukiza. Kwa kawaida tiba ya maradhi haya inachukua siku 10 hadi 20.

Miongoni mwa tiba zinazoweza kusaidia watoto kuondokana na maradhi haya ni pamoja na mkojo wa ng’ombe, kitunguu swaumu, tangawizi na Radishi.

Mkojo wa ng’ombe

Mkojo wa ng’ombe mwenye mimba ya miezi mitatu hadi mitano, uhifadhi ndani ya chupa yenye ujazo wa nusu lita, funga vizuri chupa husika. Uwe unamnywesha mtoto kijiko kimoja cha chai kutwa mara tatu. Kama mtoto ana zaidi ya miaka mitano mpe kijiko cha mezani mara tatu kwa siku.

Kitunguu swaumu

Chukua kitunguu swaumu kisage na weka ndani ya chombo kisafi, kisha ongeza maziwa kidogo, halafu koroga liwe kama tui zito la nazi, mnyweshe mtoto kijiko kimoja cha chai kutwa mara tatu, kama kasi ya mtoto kukohoa ni kubwa unaweza kuongeza kiasi cha dawa hadi vijiko sita kwa siku. Ili kuboresha radha ya dawa, unaweza kuongeza asali kidogo.

Tangawizi

Chukua tangawizi kiasi cha ujazo wa kijiko kimoja cha mezani kisha iponde au kuisaga, iweke ndani ya nusu glasi ya maji ongeza na vijiko viwili vya asali. Koroga vizuri na mpe mgonjwa anywe. Fanya hivyo mara tatu kwa siku hadi mtoto anapopata nafuu.


Radishi (mboga kama figili)

Ponda radishi, ongeza kiasi kinacholingana cha asali, koroga hadi vyote viwe vimechanganyika vizuri, kisha ongeza chumvi nyeusi kidogo na koroga tena. Mpe mgonjwa kijiko kimoja cha mezani cha dawa hiyo mara tatu kwa siku.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo au ushauri wa kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment