Tuesday, 6 March 2018

Mnyika ataka Polisi iwaambie wananchi sababu ya viongozi Chadema kuitwa huko daima

John Mnyika

Suleiman Kasei


NAIBU Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) Bara, John Mnyika amelitaka Jeshi la Polisi kuwaambia wananchi na wanachadema kuwa ni jambo gani wanatafuta kwao kwani utaratibu wa kuwaita na kuwaruhusu hautofautiani na kifungo cha nje.

Mnyika ameyasema hayo jana baada ya viongozi watano akiwemo yeye kuripoti kituoni hapo kwa mara ya tatu huku hatma ya nini wanachohojiwa ikiwa haijajulikana.

Viongozi wengine waliiotwa polisi kwa mahojiano ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Bawacha na Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko na wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mnyika amsema wao kama wabunge na viongozi wa chama wanapaswa kutekeleza majukumu mengine ya Kitaifa hivyo kitendo cha kuwaita kituoni hapo huku kukiwa hakuna kinachoondelea kinaharibu ratiba zao.

No comments:

Post a Comment