Thursday, 22 March 2018

Mpira wa wavu kuanza kutimua vumbi keshoMkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Dareva, Mawazo Lusonzo.

Asha Mwakyonde

MASHINDANO ya Ligi ya Klabu Bingwa ya mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salam yanatarajia kuanza kutimua vumbi kesho kutwa Machi 24, mwaka huu katika viwanja vimbalimbali hapa nchini.

Ligi hiyo inayoratibiwa na Chama cha Mpira wa Wavu Dar es Salaam (Dareva), itashirikisha timu  16 za wanaume na wanawake.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Dareva, Mawazo Lusonzo amesema katika mashindano hayo mshindi wa kwanza atapata Kombe na Medali.

Lusonzo ameongeza kuwa mshindi wa pili na watatu watapata medali na kwamba mashindano hayo yatafikia tamati Agosti 19, mwaka huu.

Aidha, alizitaja timu za wanaume kuwa ni City Dream, Chui, Faru, Magereza ,Jeshi Stars, Makongo, Victory Sports,Ip Sports, Mji mwema na JKT.

Lusonzo amesema timu za wanawake zitakazoshiriki ni Dar Stars, Mjimwema, Jeshi Stars, Magereza, JKT na Makongo.

No comments:

Post a Comment